Kuhusu Conrad

Mazungumzo ya ukweli — yanayobadilisha tabia.

Elimu, mazungumzo na mwongozo wenye huruma kwa afya ya akili, uponyaji wa kihisia na ukuaji binafsi.

Conrad Ley ni nani na hufanya nini?

Conrad Ley ni mkufunzi wa ustawi wa kihisia mwenye makazi yake Dar es Salaam, Tanzania. Ni mwanzilishi wa brand ya Conrad Ley na mwandishi wa audiobook “Maisha Mapya Baada ya Machozi”. Anaongoza vikao vya coaching kwa watu binafsi na wanandoa, makala za Kiswahili, na mazungumzo ya afya ya akili kwa taasisi.

Conrad ni mwanzilishi wa Conrad Ley, brand inayojikita katika kukuza afya ya akili, ustawi wa kihisia na ukuaji binafsi kupitia elimu, mazungumzo na mwongozo wenye huruma.
Dhamira Yangu

Ninaamini kwamba mabadiliko ya kudumu huanza pale mtu anapojitambua. Ndiyo sababu dhamira yangu ni kukusaidia kuelewa hisia zako, kuponya majeraha ya ndani, kujenga mahusiano yenye afya na kuishi maisha yenye amani na kusudi.

Kupitia jukwaa hili, ninashiriki na wewe maudhui yanayochochea kujitafakari na kujifunza kuhusu self-awareness, emotional healing, mental wellness, boundaries na maendeleo ya ndani kwa mtazamo usiohukumu.

Lengo si kutoa majibu ya haraka, bali kukupa maarifa na zana zinazoweza kukusaidia kufanya mabadiliko ya kweli katika maisha yako.

Brand Imejengwa Juu ya
UkweliHurumaUtulivuUsalama wa Kihisia

Ninaamini kila mtu anastahili nafasi ya kusikilizwa, kueleweka na kukua bila kuhukumiwa.

Kadiri safari hii inavyoendelea, maono yangu ni kujenga jamii yenye uelewa mpana kuhusu afya ya akili kupitia:

  • Coaching ya mtu mmoja mmoja
  • Programu za vikundi
  • Retreats za ustawi wa akili
  • Mazungumzo ya wellness kwa taasisi na mashirika

Asante kwa kuwa sehemu ya safari hii.

Natumaini jukwaa hili litakuwa mahali ambapo utajifunza zaidi kuhusu wewe mwenyewe, utapata ujasiri wa kukabiliana na changamoto zako, na utaendelea kujenga maisha yenye afya, amani na maana.

— Conrad Ley
Conrad Ley
#njootuzungumze
Jiunge

Pokea ushauri wa kila wiki.

Reflections, vipindi vipya, na zana za kukusaidia kuelewa akili yako — moja kwa moja kwenye inbox yako.

conradley.
Talk About It With Conradley © 2026. Badilisha Tabia, Badilisha Maisha.Imeundwa kwa upendo · Tanzania