Maswali

Maswali yanayoulizwa mara kwa mara.

Majibu mafupi, ya moja kwa moja kuhusu huduma, bei, na jinsi ya kuanza.

Conrad Ley hutoa nini, na kwa bei gani?

Conrad Ley anafanya coaching ya ustawi wa kihisia, makala, na vitabu vya sauti. Vikao huanzia TZS 45,000 kwa Online Session hadi TZS 200,000 kwa Couple Session, na audiobook “Maisha Mapya Baada ya Machozi” inauzwa TZS 25,000 kwa malipo ya mara moja.

Jukwaa linahusika na nini?

Hili ni jukwaa la Kiswahili linaloendeshwa na Conrad Ley, likitoa mazungumzo, makala na vitabu vya sauti kuhusu saikolojia ya mahusiano, afya ya akili na ukuaji binafsi. Jukwaa linafanya kazi kutokea Dar es Salaam, Tanzania, na hutoa vikao mtandaoni na ana kwa ana.

Conrad Ley ni nani?

Conrad Ley ni mkufunzi wa ustawi wa kihisia mwenye makazi yake Dar es Salaam, Tanzania. Anaongoza mazungumzo ya afya ya akili kwa Kiswahili, huendesha vikao vya coaching vya mtu mmoja mmoja na wanandoa, na ni mwandishi wa audiobook ya "Maisha Mapya Baada ya Machozi".

Vikao vya Conrad Ley vinagharimu kiasi gani?

Online Session inagharimu TZS 45,000. One on One inagharimu TZS 120,000. Couple Session inagharimu TZS 150,000 hadi TZS 200,000. Kikao cha Bonus kinacho jumuisha vikao vitatu kwa discount kinagharimu TZS 110,000. Malipo hufanyika baada ya kuthibitisha nafasi kupitia social media DMs na WhatsApp.

Audiobook "Maisha Mapya Baada ya Machozi" inagharimu kiasi gani?

Audiobook inauzwa kwa TZS 25,000 tu, ambayo ni malipo ya mara moja. Baada ya malipo unapata ufikiaji wa kudumu wa sura zote 9 ndani ya akaunti yako, bila ada ya kila mwezi.

Audiobook ina sura ngapi na ni ya lugha gani?

Ina sura 9 zilizorekodiwa kwa Kiswahili, zikianzia na "Mwanamke Aliyejisahau". Kila sura inasikilizwa kupitia kicheza sauti cha tovuti. Unaweza kusikiliza dondoo la sekunde 30 bure kabla ya kununua.

Ninawezaje kuweka nafasi ya kikao?

Nenda ukurasa wa Weka Nafasi, chagua aina ya kikao, jaza fomu fupi, kisha utaelekezwa WhatsApp kwa namba +255 768 373 143 kuthibitisha muda. Majibu hutolewa ndani ya saa chache za siku za kazi.

Vikao vinafanyika mtandaoni au ana kwa ana?

Vyote viwili. Online Session hufanyika kwa video au simu popote ulipo. Vikao vya ana kwa ana hufanyika Dar es Salaam, Tanzania, kwa makubaliano ya mahali na muda.

Je, huduma hii ni matibabu ya kisaikolojia au kiakili (Therapy)?

Ndiyo. Huduma hizi zinatoa ushauri na msaada wa kisaikolojia (Therapy) ili kukusaidia kukabiliana na changamoto mbalimbali za kihisia, mahusiano, na mfumo wa maisha kwa njia za kitaalamu.

Naweza kupata maudhui gani bure?

Makala na nukuu kwenye ukurasa wa Makala & Nukuu ni bure, pamoja na dondoo la audiobook la sekunde 30 na maudhui yanayochapishwa kwenye Instagram @talkboutitwithconradley.

Ninawasilianaje na Conrad Ley?

Njia ya haraka ni WhatsApp: +255 768 373 143. Unaweza pia kutumia fomu kwenye ukurasa wa Wasiliana au kutuma ujumbe Instagram, Facebook na Tiktok @conradley.

Jiunge

Pokea ushauri wa kila wiki.

Reflections, vipindi vipya, na zana za kukusaidia kuelewa akili yako — moja kwa moja kwenye inbox yako.

conradley.
Talk About It With Conradley © 2026. Badilisha Tabia, Badilisha Maisha.Imeundwa kwa upendo · Tanzania